Steve RnB amekiri kutokuwa na maelewano na mtayarishaji wa muziki aliyemtambulisha kwenye orodha ‘A’ ya muziki nchini, Man Walter.

Msanii huyo ambaye hakuwa tayari kueleza kwa undani kuhusu chanzo cha kutoelewana kwao alisema kuwa yaliyotokea kati yao yamesamsababisha kushindwa kusogea katika maeneo ya studio za Combination Sound zinazomilikiwa na Man Walter.

Ingawa hakueleza chanzo, taarifa za watu wa karibu wa wawili hao zimeeleza kuwa chanzo ni kupishana katika biashara ya tangazo na kwamba msanii huyo anaamini alidhurumiwa pesa kwenye biashara hiyo.

“Man Water na mimi tulikuwa na misunderstand (kutoelewana) ambako kulitokea huko nyuma, lakini sasa hivi nadhani wote tayari tumesahau yaliyotokea,” aliiambia East Africa Television. “Kabla ya hayo mambo tulikuwa  tunafanya kazi kama brothers (ndugu),” aliongeza.

Alisema ingawa kumekuwa na hali hiyo kati yao, bado anaheshimu mchango wa mtayarishaji huyo na anamchukulia kama kaka yake na mtu aliyemtambulisha kwenye ulimwengu wa Bongo Fleva.

Isco kubaki Santiago Bernabeu mpaka 2022
Madam Rita kuirejesha ‘Bongo Star Search’ kwa kishindo