Aliyekua nahodha na kiungo wa klabu ya Liverpool Steven Gerrard ametangaza kustaafu soka.

Gerrard ametangaza maamuzi hayo, baada ta kuutumikia mchezo wa soka ngazi ya timu za wakubwa kwa miaka 19.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 36, amefikai maamuzi hayo ikiwa ni baada ya kumalizana kimkataba na klabu ya LA Galaxy ya Marekani ambayo alianza kuitumikia mwaka 2015.

Asilimia kubwa ya maisha ya soka ya Gerrard, yalikua kwenye klabu ya Liverpool ambayo aliitumikia katika michezo 710 na kufunga mabao 120.

Gerrard alianza kuitumikia klabu hiyo ya Anfield mwaka 1998 akipandishwa katika kikosi cha wakubwa, baada ya kunolewa kwa muda mrefu kwenye kituo cha kukuza vipaji cha klabu hiyo tangu mwaka 1987.

Mwaka 2015 aliondoka klabuni hapo na kutimkia nchini Marekani kucheza ligi ya nchi hiyo MLS, ambapo akiwa na LA Galaxy alifunga mabao 5 katika mapambano 34 aliyocheza.

Video: DC Lyaniva aitaja mikakati kuiboresha Temeke
Giampiero Ventura Asikia Kilio Cha Balotelli