Mshambuliaji wa klabu ya Everton Steven Naismith anatarajiwa kujiunga na Norwich City mwezi Januari kwa dau la pauni milioni 8.

Naismith mwenye umri wa miaka 29 amecheza michezo minne tu katika msimu huu wa ligi kuu England, lakini akiwa kafunga hat-trick kwenye mchezo dhidi ya Chelsea .

Mwanzo wa wiki mchezaji huyu alicheza kwa dakika 25 katika mchezo ambao Everton walilala kwa mabao 4-3 dhidi ya Stoke City.

Wakati wa dirisha kubwa la usajili la mwezi August Everton waliweka dau la pauni 7, Mshambuliaji huyu ameichezea timu yake jumla ya michezo 103 na kufunga magoli 18 toka aliposajiliwa kutoka Rangers ya Usikoch.

Naibu Waziri Aagiza Kutimuliwa Kazi Raia wa Kigeni Kwenye Makampuni ya Simu Kwa Kikiuka Sheria
Bamford Aubomoa Mkataba Wa Crystal Palace

Comments

comments