Klabu ya AFC Leopards imetangaza kumsaini kocha wa zamani wa Azam FC Stewart Hall kwa mkataba wa miaka miwili kama kocha mkuu.

Stewart amepata dili hilo akiwapiku Sam Timbe, Didier Homes Da Rosa, Mnyarwanda Andrew Mbungo, Mfaransa Patrick Liewig pamoja na Mserbia Popadic Dragan.

Kwenye ngazi ya vilabu, Stewart Hall amezifundisha Pune FC ya India na Sofapaka inayoshiriki ligi kuu ya Kenya (Kenyan Premier League) kabla ya kujiunga na Azam FC.

Mwaka 2015 Hall alikiongoza kikosi cha Azam FC kutwaa taji la CECAFA Kagame Club Cup baada ya kuifunga Gor Mahia 2-0 katika mchezo wa fainali ulipigwa jijini Dar es Salaam.

AFC Leopards ilimtimua kocha wake raia wa Ubelgiji Ivan Minnaert mwezi September kwa kile kilichodaiwa ni kiwango kidogo. Ezekiel Akwana na Nicholas Muyoti wakakabidhiwa majukumu ya kuinoa timu kwa muda.

“Tumesitisha mkataba mara moja, Kama unakumbuka wakati Minnaert anaingia kuchukua timu tulikuwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi lakini kwa sasa tupo nafasi ya 10. Tupo nje ya GOtv Shield na nafasi ya nane kwahiyo hadi tunavyoongea, hatuna uhakika kama tutashuka daraja au tutasalia kwenye ligi,” anasema Mwenyekiti wa AFC Leoprds Mule.

Waamuzi Wa Bongo Wamvuruga Zeben Hernandez
Selfie Za Wachezaji Wa Arsenal Zawakera Magwiji