Papa Francis amesema kuwa mapenzi ya jinsia moja kwa makasisi ni jambo kubwa na ambalo limekuwa likimpa hofu kubwa.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani ametoa kauli hiyo katika mahojiano na Mmishenari kutoka Uhispania kuhusu wito wa kidini.

Mahojiano hayo ni sehemu ya kitabu kinachoandikwa na mmishenari huyo kuhusu masuala mbalimbali ya kidini.

Aidha, Papa amesema kuwa mahusiano ya jinsia moja ni jambo la “fasheni”, na ametaka makasisi kutii viapo vyao vya utawa kutojihusisha na mapenzi.

Gazeti la Corriere della Sera la nchini Italia limechapisha sehemu ya mahojiano hayo katika mtandao wake juzi Jumamosi.

“Hili suala la mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja ni kubwa sana, wale wote wanaohusika na mafunzo kwa makasisi wahakikishe kuwa wanafunzi wao wamekomaa kibinaadamu na kihisia kabla ya kuwapatia Sakramenti ya Upadre (upadrisho), amesema Papa Francis

Hata hivyo, mwaka 2013, Papa alisisitiza juu ya msimamo wa Kanisa hilo kuwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja ni dhambi na haikubaliki.

 

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro avunja Bodi ya Benki ya Ushirika (KCBL)
Maelfu ya watu wakusanyika kumuenzi Mandela

Comments

comments