Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ametaka Rais Dkt. Magufuli apewe muda kwanza wa kunyoosha na kurejesha misingi ya utaifa kabla hajagusa kwenye suala la mchakato wa Katiba Mpya.

Polepole ametoa kauli katika ukurasa wake wa twitter ambapo amesema kuwa yeye hakuwahi kusema Katiba inayopendekezwa ni nzuri hivyo rais anapaswa kupewa muda wa kuimarisha nchi na Ukatiba.

“Aliyesema Katiba Inayopendekezwa nzuri nani? Ilipatikana bila muafaka, maridhiano na uelewa wa pamoja. Tumpe nafasi Ndg. Magufuli atunyooshe, aturejeshee misingi ya Utaifa, hasa nidhamu ya sisi viongozi na umuhimu wa kuheshimu watu. Saizi tujenge nchi na kuimarisha UKATIBA,”ameandika Polepole

Aidha, Oktoba, 2014 Bunge maalum la Katiba nchini Tanzania lilipitisha rasimu ya katiba iliyopendekezwa ambapo kabla ya kupitishwa kwa rasimu hiyo, bunge hilo maalum lilikaa kama kamati kujadili mapendekezo katika Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na tume hiyo ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya uongozi wa Jaji Joseph Warioba.

Mahakama yaitaka Serikali kuhakikisha Miguna anafika mahakamani
Subirini kwanza JPM atunyooshe- Polepole