Serikali ya Sudani kusini imepanga kuzifunga baadhi ya balozi zake kwaajili ya kubana matumizi zikiwemo balozi za Norway na Ufaransa.

Serikali ya mjini Juba imesema uamuzi wake huo ni kutokana na kuzorota kwa uchumi katika nchi yao huku bado ikiendelea kukabiliwa na ukosefu wa utulivu wa kisiasa.

Msemaji wa mambo ya nje, Mawien Makol amesema kwamba Sudan kusini imechukua hatua ya kufunga baadhi ya balozi zake katika nchi za Ufaransa, Norway, Ghana, Kuwait na Italia.

Makol amesema wameamua kujaribu kufanya matumizi ya bajeti ya nchi yao kwa busara kulingana na uwezo wa nchi hiyo kwa kuwa wanagharamia balozi zao kutokana na rasilimali za nchi pamoja na fedha za misaada ya kuunga mkono mipango ya ujenzi baada ya nchi hiyo kutoka kwenye Migogoro.

Mnamo mwezi mei 2019, umoja wa mataifa uliongeza vikwazo vya silaha na dhidi ya maafisa kadhaa baada ya kuzuka mapigano mapya.

Ikumbukwe kuwa Ufaranza ina kura turufu katika jumuiya ya kimataifa na inaweza kutumia nguvu yake katika Baraza la usalama kushinikiza Sudan kusini hatua ambayo siyo njema kwa serikali ya Juba.

Wachambuzi wa kisiasa wamesema kuwa kufungwa kwa balozi za Sudan kusini kunaweza kuipunguzia nafasi nchi hiyo kwenye medani za kidiplomasia .

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 16, 2019
Ali Kiba afunguka wasanii Bongo kutotajwa Tuzo za BET 2019