Aliyekuwa Rais wa Sudan na kuondolewa kwa nguvu madarakani na Jeshi la nchi hiyo mwezi Aprili mwaka huu, Omar al-Bashir ameshtakiwa kwa kosa la ufisadi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya mwendesha mashtaka imeeleza kwaufupi kuwa Bashir ameshtakiwa kwa makosa yanayohisiana na sheria zinazo husu utajiri haramu na maagizo ya dharura.

Tokea alipo pinduliwa na kukamatwa baada ya kutawala miaka 30 hajawahi kuonekana kwa umma licha ya kuwa anakabiliwa na kesi lukuki, ikiwemo ya kuchochea na kuhusika na mauaji ya waandamanaji aliyoshtakiwa mwezi mei baada ya uchunguzi uliofanywa kuhusu kifo cha daktari aliyeuawa wakati wa maandamano yaliyopelekea kumalizika kwa utawala wake.

Hata hivyo hatima ya Bashir haijawekwa wazi, aliripotiwa kutiwa nguvuni mara baada ya kupinduliwa kutokana na maandamano dhidi ya uamuzi wa serikali yake kupandisha mara tatu bei ya mkate, yaliyoanza mwezi disemba mwaka jana na kudumu kwa wiki tano.

Licha ya Bashir kuondoka madarakani bado kuna ghasia za waandamanaji wanaodai demokrasia ambazo tayari zimepelekea vifo vya watu 61 kwa mujibu wa maafisa na 118 kwa mujibu wa madaktari wanaounga mkono waandamanaji hao.

Msemaji wa jeshi amekiri makosa kufanyika wakati majenerali walipo amrisha kumalizika kwa mgomo wa kukaa mbele ya makao makuu ya jeshi ambapo waandamanaji wanadai kurejeshwa kwa utawala wa kiraia nchini humo.

Mazungumzo baina ya waandamanaji na baraza la kijeshi la mpito yalivunjika baada ya ghasia, japo viongozi wa maandamano baadae waliyaita maandamano hayo kuwa ni ukaidi wa raia ambayo hayanabudi kukoma ili kufufuliwa kwa mazungumzo ya amani.

Jeshi limesema kuwa linamatumaini Marekani inaweza kuwa na mchango mzuri baada ya mkutano baina ya Tibor Nagy, naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayehusika na masuala ya Afrika na Luteni Jenerali Abdel Fattah al – Burhan.

Ikumbukwe kuwa Omar al-Bashir, aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1989 na ameliongoza taifa hilo lililokuwa kubwa zaidi barani Afrika hadi mwaka 2011 alipochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia, ambapo Sudan ilikuwa katika mwaka wa 21 wa mapigano makali ya wenyewe kwa wenyewe kati ya kaskazini na Kusini.

Kabla ya Bajeti kusomwa Kenya, Wabunge wanawake walisusia kikao
LIVE: Rais Tshisekedi wa DRC Congo atembelea Bandari ya Dar es salaam

Comments

comments