Nchi ya Sudan, Itakua mwenyeji wa michuano ya Kombe la CECAFA kwa mwaka huu, baada ya baraza la vyama vya soka Afrika mashariki kuthibitisha.

Kwa mara ya mwisho Sudan ilikua mwenyeji wa michuano ya CECAFA mwaka 2013.

Nchi ya Uganda nayo imeteuliwa kuwa mwenyeji wa michuano ya wachezaji chini ya umri wa miaka 17 yaani (CECAFA Under-17) na pia michuano ya ubingwa upande wa wanawake mwaka huu.

Burundi itakuwa mwenyeji wa fainali za wachezaji wa chini ya miaka 20.

CECAFA pia imetangaza mpango wa miaka mitano ambao utasisitiza ukuaji wa soka kwa vijana upande wa wanawake pamoja na kuimarisha uwezo wa kiufundi.

Hayo yakijiri, rais wa Shirikisho la Soka la Somalia Abdiqani Said Arab ameteuliwa kuwa naibu mwenyekiti wa Cecafa.

 

JKT Ruvu Wawavutia Kasi Maafande Wenzao
Rooney Atwaa Tuzo England