Marekani imerejesha kile kinachoitwa kinga ya mamlaka ya Sudan, baada ya baraza la Congress kupitisha sheria ya kurasimisha hatua hiyo kufuatia Sudan kuondolewa kwenye orodha ya mataifa yenye kufadhili ugaidi.

Nchi hiyo iliyokuwa kwenye orodha ya mataifa yenye kufadhili ugaidi kwa karibu miongo mitatu, imeathirika pakubwa kiuchumi kutokana na kuwekewa vikwazo vya kupokea misaada.

Kuondolewa kwenye orodha hiyo pia kumewaletea nafuu kubwa wawekezaji.

Sudan ilikuwa inafanya mazungumzo na Marekani kwa miezi kadhaa sasa, na kukubali kulipa dola za Kimarekani Milioni 335 kwa waathiriwa wa mashambulio ya Al-Qaeda yaliyolenga Balozi za Marekani katika ukanda wa Afrika Mashariki mnamo mwaka 1998.

Nchi hiyo sasa ina matumaini pia ya kuanzisha tena mahusiano ya kidiplomasia na Israel pamoja na nchi nyingine za Kiarabu.

Mabasi 16 yaonywa uvunjifu wa sheria
Ummy,Maalim Seif wateta jambo