Zaidi ya watu Sabini wamefariki dunia kutokana na mafuriko yaliyoikumba nchi ya Sudan, na kusababisha uharibifu wa mali na nyumba kuzama.
 
Habari kutoka nchini humo  zinaeleza kuwa hayo ni mafuriko mabaya zaidi  kuwahi kuikumba Sudan, ambapo tayari nchi hiyo imeomba msaada wa kimataifa wa  kukabiliana na idadi kubwa ya watu wanaohitaji misaada mbalimbali.
 
Serikali ya Sudan imesema imejaribu kusambaza misaada kadhaa kwa wahitaji lakini haitoshi, kwani wengi bado hawajafikiwa na misaada hiyo.

Baadhi ya watu walioyakimbia makazi yao baada ya nyumba zao kuharibiwa na mafuriko hayo wameilaumu Serikali kwa kushindwa kuwapatia misaada, na  hivyo kufanya maisha yao kuwa hatarini.
 
Vijiji vipatavyo hamsini vimeharibiwa na mafuriko hayo yaliyoyakumba majimbo manane katika nchi hiyo ya Sudan.

Kingo za mto Nile wenye matawi yake nchini Sudan zimepasuka baada ya kuzidiwa na maji, ambapo maji hayo yamekuwa yakiingia kwenye makazi ya watu.

Afghanistan:Sheria mpya kwa wanafunzi wa kike
Saba wawania Udiwani CCM Kata ya Ndembezi