Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyassa, Emmanuel Masonga wamerudishwa rumande hadi Januari 22, 2018 siku ya Jumatatu ambapo kesi yake itaanza kusomwa mfululizo.

Wawili hao wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kutenda kosa la uchochezi katika mkutano wao wa hadhara ambao ulifanyika Disemba 31, 2017 jijini Mbeya ambapo jeshi la polisi limesema kuwa viongozi hao walizungumza maneno yenye kuleta chuki kati ya Serikali na wananchi.

Aidha, January 16, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Jijini Mbeya iliamuru Mbunge huyo na mwenzake wapelekwe rumande kwa tuhuma za kesi ya uchochezi.

Hata hivyo, Viongozi hao wamerudishwa rumande tena mpaka siku ya Jumatatu ambapo kesi yao itaanza kusomwa tena.

 

Majaliwa apiga marufuku kilimo cha mkataba
Chadema wamtaja mgombea Kinondoni