Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Mbilinyi amesema kuwa wadau wengi hawajitokezi kusaidia kwenye masuala ya elimu kutokana na sera ya elimu bure ambayo imepelekea serikali kufuta ada.

Sugu amesema kuwa fedha anazopata kupitia muziki wake amekuwa akisomesha zaidi ya wanafunzi 400 katika kituo cha watoto anachokilea, hivyo ameomba msaada kutoka kwa wadau wajitokeze ili kusaidia elimu.

Amesema kuwa miaka ya nyuma kabla ya elimu bure alikuwa akiwalipia ada japo kwasasa hategemei sana muziki na kwamba anavyanzo vingine anavyo vitegemea.

“Bahati mbaya sasa hivi kutokana na sera ya elimu bure, mashirika na taasisi nyingi hawajitokezi kusaidia kwani wataonekana wanaenda kinyume na sera ya elimu bure, lakini kiuhalisia wamefuta ada tu ila bado kuna uhitaji mkubwa sana hasa kwa watoto wenye uhitaji maalum hivyo amewaomba wadau kujitokeza.

Hata hivyo Sugu ni miongoni mwa wasanii ambao wamefanikiwa kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Akiwa sambamba na Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay  ambaye aliingia katika siasa na kufanikiwa kushinda ubunge kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Gutteres azitaka Israel na Hamas kusitisha mapigano
Serikali yataifisha tani 240 za Mahindi na kuzigawa