Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia ni msanii wa muziki wa bongo fleva, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amewataka watu mbalimbali wakiwemo askari wa jeshi la magereza kumtumia picha akiwa amevaa sare za jela.

Sugu amesema kuwa muitikio umekuwa mkubwa lakini bado hajaipata picha husika, na kusisitiza mtu yeyote atakayeipata picha hiyo amtumie kwa email na atapewa zawadi yake, huku akiahidi kuweka usiri mkubwa kati yao.

“Kwa kweli bado mpaka sasa hivi sijampata, najua wanakataza kupiga picha jela ndio maana nimetoa tangazo kama kuna mtu anayo, na sitamtaja, na ndio maana tunataka kwa njia ya email, ninachotaka ni picha kwa ajili ya kukamilisha kitabu chetu”, amesema Sugu.

Aidha, Sugu ameendelea kwa kusema kuwa muitikio umekuwa ni mkubwa lakini picha bado hajaipata, ambapo amesema watu wanataka kushiriki katika kukamilisha kitabu chake.

Hata hivyo, hivi karibuni Mbunge huyo aliandika ujumbe mfupi kwenye ukurasa wake wa Twitter akimtaka mtu mwenye picha yake akiwa amevaa sare za jela amtumie kwa ajili ya kumalizia kurasa ya mwisho ‘cover’ ya kitabu chake cha ‘SIASA NA MAISHA, na kuahidi kumpatia kiasi cha sh milioni 1 yeyote atakayefanikisha kuipata picha hiyo.

 

Boko Haram wavamia vijiji, wafanya mauaji
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 22, 2018