Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa CHADEMA Nyanda ya Juu Kusini, Emmanuel Masonga, wameachiwa huru.

Walifungwa katika Gereza la Ruanda Jijini Mbeya walikokuwa wakitumikia kifungo cha miezi (5) baada ya kukutwa na hatia ya Uchochezi.

Hukumu hiyo ilitolewa Februari 26 mwaka huu jijini Meya na walishtakiwa kwa tuhuma za kutoa lugha za uchochezi katika mkutano wa hadhara.

Trump aionya Iran kuhusu Nyuklia
Aliyeolewa mara 11 auawa kwa kupigwa Mawe

Comments

comments