Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mbeya imewahukumu kifungo cha miezi mitano jela, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu, Emmanuel Masonga.

Wanasiasa hao wamehukumiwa kifungo hicho leo baada ya kukutwa na hatia ya kufanya kosa la kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite.

Sugu na Masonga ambao walikuwa wakitetewa na wakili Peter Kibatala, walidaiwa kutenda kosa hilo Disemba mwaka jana katika mkutano wa hadhara jijini Mbeya.

Shyrose akanusha kumponda JPM
Raia kupewa pesa zilizobaki bajeti ya 2017