Wavuvi 12 wameuawa na viboko na wengine 15 wamejeruhiwa na wanyama hao, wakati wakivua samaki ndani ya bwawa la Mtera katika kipindi cha mwaka mmoja.

Kufuatia kuongezeka kwa matukio hayo, Kamanda wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori nchini (TAWA) Nyanda za Juu Kusini Kamishna Msaidizi Joas Makwati amesema, TAWA itapeleka .boti ya doria ili.kudhibiti wanyama hao.

Naye Mkuu wa wilaya ya Iringa, Mohamed Moyo amewambelea wavuvi wanaofanya shughuli za uvuvi katika bwawa la Mtera kwa lengo la kuwapa pole na kuwataka kuzingatia usalama wao wawapo kazini.

Aidha Moyo Amewaagiza maafisa Uvuvi, viongozi wa Serikali kwa ngazi zote kusimamia na  kuhamasisha njia bora za uvuvi katika Bwawa la Mtera ili kuepuka migongano ya Wanyama pori wakali na waharibifu akisisitiza kufuata miongozo na kanuni za uvuvi.

Pia ameitaka TAWA kuongeza nguvu katika kuwadhibiti viboko, ili wasiendelee kuleta madhara.

Manara: Hatujapata ITC zao mpaka sasa
RC Makalla apiga marufuku wamachinga kufanya biashara njia za watembea miguu