Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu akimnadi mgombea urais kwa tiketi ya Chadema anaeungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa, ameeleza nafasi atakayokuwa nayo baada ya uchaguzi.

Akiongea katika mahojiano maaalum na Tido Mhando wa Azam TV, Sumaye alieleza kuwa hajaahidiwa cheo chochote na upande wa upinzani na kwamba uamuzi wake wa kuwasaidia ni kutaka kuongeza nguvu zaidi ya uzoefu katika kuleta mabadiliko nchini.

Alisema kuwa ameamua kuwa mwanaharakati kama Ernesto ‘Che Guevara ‘de la Serna, aliyefanya kazi ya kuleta mapinduzi katika nchi mbalimbali ikiwemo nchi ya Cuba.

“Kwa sasa ninafanya kazi kama Che Guevara, nadhani hii ni nafasi muhimu zaidi hasa kama hao watu watautumia ushauri wako,” alisema.

Fred Sumaye

Sumaye alieleza kuridhishwa na kazi wanayoifanya Ukawa kwa kuwa wameibua upinzani mkali dhidi ya CCM. Ingawa alisisitiza kuwa na uhakika kuwa Ukawa watashinda katika uchaguzi huu kwa jinsi alivyoshuhudiwa wananchi wengi wanaouunga mkono umoja huo, Sumaye alieleza kuwa endapo hawatashinda bado watakuwa wamefanya kazi kubwa kwa kuwa serikali ya CCM itakayoingia madarakani haitalala tena. Alisema upinzani waliokutana nao mwaka huu utaiamsha CCM.

Sumaye alitangaza kujiunga na kambi ya Ukawa akitokea CCM na kueleza kuwa amechukua uamuzi huo kwa nia ya kuongeza nguvu ya kuleta mabadiliko.

Mwarabu Wa PSG Amtengea Fungu Ronaldo
Emmanuel Mbasha Ashinda Kesi Ya Ubakaji