Mwenyekiti wa CHADEMA, Kanda ya Pwani, Fredrick Sumaye, amesema kuwa yapo mashinikizo mbalimbali yanayowataka viongozi waliotoka Chama Cha Mapinduzi na kuhamia Upinzani warudi ndani ya Chama hicho huku akibainisha kuwa vitendo vingine wanavyofanyiwa ni vya kuwaumiza.

Amesema kuwa wapo watu wanaowafuata na kuwapelekea maneno, na hata kutendewa mambo mbalimbali ya lakini yeye bado ameendelea kuwa na msimamo wake wa kuwa upinzani na ataendelea kuvumilia.

“Mimi nilipotoka CCM nilitoka kwa hiari yangu. Siwezi kurudi kwa kushurutishwa na mtu yeyote. Siyo maneno tu yanayotutaka turudi huko, bali yapo mambo mengi tunatendewa ili turudi lakini kila mtu ana uamuzi wake. Kama una maamuzi yako imara hata kama utatendewa mambo fulani fulani utasimama na misimamo yako huku unaumia”, ameema Sumaye.

Aidha amesema kuwa Lowassa alikwenda CHADEMA baada ya kuonekana kwamba ameonewa CCM, lakini siyo kwamba walikikuta hakuna mafanikio ndani ya chama hicho cha upinzani, huku akisema mafuriko kipindi cha uchaguzi hayakusababishwa na Lowassa.

Hata hivyo, ameongeza kwamba watu walishaichoka CCM tangu 2010 wakataka mabadiliko lakini hata sasa watataka mabadiliko sana, kuondoka kwa Lowassa hakuwezi kusababisha pengo ndani ya Chadema.

Magufuli awashangaa Polisi kutekwa Mo Dewji, ‘Watanzania sio wajinga’
Neema Mgaya atumia Milioni 144.5 kuunga mkono shughuli za maendeleo mkoani Njombe