Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Nigeria, Sunday Oliseh ametangaza kujizulu nafasi hiyo, ikiwa ni baada ya miezi minne tangu alipoajiriwa na shirikisho la soka nchini humo NFF.

Oliseh ambaye aliwahi kuwa nahodha wa kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria (Super Eagles), amefikia maamuzi hayo kutokana na kucheleweshewa malipo ya mshahara wake.

Hata hivyo mpaka sasa uongozi wa shirikisho la soka nchini Nigeria, bado haujatoa tamko lolote kuhusu maamuzi yaliyochukuliwa na kocha mkuu wa timu ya taifa, ambayo ipo katika harakati za kusaka nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 pamoja na fainali za kombe la Afrika za mwaka 2017.

Oliseh, amechukua maamuzi ya kutangaza kujiondoa katika nafasi ya ukocha wa Super Eagles, kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kwa kuamini ni njia rahisi kwake kuwafikishia ujumbe mashabiki wa soka duniani kote.

Magufuli awapa saa nne mawaziri wake, vinginevyo watakuwa wamejitumbua jipu
Rais Wa Nigeria Atimiza Ahadi Baada Ya Miaka 30