Klabu ya Sunderland imefanikiwa kumrejesha Emmanuel Eboue, katika ligi ya nchini England, baada ya kumsajili kama mchezaji huru.

Eboue ambaye aliondoka nchini England mwaka 2011 baada ya kuuzwa na klabu ya Arsenal kwenye klabu ya Galatasaray, ya nchini Uturuki, amejiunga na The Black Cats, hadi mwishoni mwa msimu huu.

Kabla ya kukamilisha usajili wa klabu ya Sunderland, beki huyo wa pembeni mwenye umri wa miaka 32, alikua akifanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha klabu hiyo ambayo inahaha kujiondoa kwenye mkia wa kushuka daraja msimu huu.

Eboue, aliachwa na klabu ya Galatasaray mwishoni mwa msimu uliopita, kufuatia baadhi ya mambo kutokwenda sawa kati yake na viongozi wa klabu hiyo, ambayo imekua katika ushindani mzuri kwenye msimamo wa ligi ya nchini Uturuki.

Akiwa nchini Uturuki Eboue, alifanikiwa kutwaa mataji ya ligi ya nchini humo mara tatu, hali ambayo inatazamwa kama kichocheo cha kuleta chachu kwenye kikosi cha Sunderland ambacho kinaamini kitasalia kwenye ligi kuu nchini England kwa ajili ya msimu ujao wa 2016-17.

Vijana 6 Wa Zenji Wa Shotokan Karate Kupigwa Msasa Dar es Salam
Zoezi La Kusaka Suluhu Lashindikana