Kiungo wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amewaita Mashabiki na Wanachama wa Young Africans Uwanja wa Mkapa kesho Jumamosi (Agosti 13), ili kuipa nguvu timu yao.

Young Africans itacheza dhidi ya Simba SC kwa mara ya kwanza msimu wa 2022/23, ikitetea Ngao ya Jamii iliyoitwaa msimu uliopita kwa kumfunga Mnyama bao 1-0.

Sure Boy amesema baada ya kupoteza mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Mabingwa wa Uganda Vipers SC, Kikosi chao kimejiandaa na kujizatiti kwa mpambano dhidi ya Simba SC, huku akinadi wana Kikosi Bora na Imara.

Amesema kila mchezaji wa Young Africans anatambua umuhimu wa kutwaa Mataji, baada ya kufanya hivyo msimu uliopita kwa kutwaa Mataji Matatu, hivyo kesho Juamamosi watapambana ili kutetea kilicho halali kwao.

“Tuna kikosi Bora na cha ushindani, maandalizi yanakwenda vizuri kila mhezaji amejiandaa kuhakikisha anashinda mchezo wa Kesho Jumamosi, ili kuendeleza pale tulipoishia,”

“Kupoteza mchezo wetu wa Kirafiki dhidi ya Vipers SC kumetuongezea chachu ya ushindani, mashabiki njooni kwa wingi Uwanja wa Mkapa, tutawafurahisha kesho Jumamosi”

Kitu Kikubwa nadhani kila mtu anaelewa Ukubwa na Presha ya mchezo wa Dabi inavyokuwa kwa sababu kila upande umekuwa ukitafuta matokeo ili kuwa katika nafasi nzuri kwenye ushindani na mshindi kwenye mchezo huo ni Bingwa, hakuna asiyetaka taji la Ngao ya Jamii Kesho Jumamosi.” amesema Sure Boy

Simba SC ina deni la kulipa kisasi cha kufungwa na Young Africans msimu uliopita, wakipoteza mchezo wa Ngao ya Jamii kwa 1-0 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, pia walikutana na matokeo hayo Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza katika mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.

Kenya: Fomu 34A, 34B na 34C ni nini?
Fei Toto, Aziz Ki wamtisha Mtemi Ramadhan