Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameshindwa kujizuia na kuhoji muonekano wa Suti ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi kwa kutaka kufahamu kwa nini pamoja na kuvaa suti nzuri lakini bado zinaonekana na namba ambazo hazieleweki.

Amehoji hayo wakati Mbunge huyo akitoa mchango wake katika bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa fedha 2018/19.

“Kabla sijakuongezea dakika moja waheshimiwa wengi wameniandikia kwamba umevaa suti nzuri sana lakini umeweka lebo za ajabu hiyo 219 ni kitu gani?,”amehoji Spika Ndugai

Aidha, katika majibu yake, Ugu amesema kuwa hiyo ni namba yake ya mfungwa wa jela, ambayo ataendelea kuvaa kadiri ambavyo atajisikia. huku akisema kuvaa suti kali ni kawaida yake.

Hata hivyo, Mbunge huyo kutoka Mbeya Mjini amekuwa akionekana akivaa nguo zenye namba 219 mbele ambapo huwa akifafanua kuwa ilikuwa namba yake siku alipoingia Gereza la Ruanda baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezi 5 kwa kosa la kutoa lugha chafu dhidi ya Rais Dkt. Magufuli

Rosa Ree afunguka kuhusu mistari ya Chemical ‘inayomkwaruza’
Mdee adai ni aibu kufundishwa na Prof. Kabudi