Wakati Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, wakitarajia kuanza maandalizi ya kuelekea mchezo wa mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar, Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck amefunguka ugumu aliokutana nao wakati wa mchezo wa ufunguzi dhidi ya Ihefu FC.

Simba walinzia jijini Mbeya mwishoni mwa juma lililopita kwa kupata ushindi dhidi ya timu hiyo ambayo inashirii kwa mara ya kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini walikutana na wakati mgumu wa kutimiza lengo la kuambulia alama tatu muhimu.

Kocha Sven amesema mchezo huo uliounguruma kwenye Uwanja wa Sokoine, ulikua mgumu na haikua kazi rahisi kwa wachezaji wake kufanikisha lengo la ushindi, kama mashabiki wengi wanavyodhani.

Kocha huyo kutoka nchini Ubelgiji amesema kabla ya mchezo huo alizungumza na wachezaji wake na kueleza namna ambavyo mpambano huo ungekua, na ndivyo ilivyoonekana wakati wote wa dakika 90.

“Nilijua mchezo itakuwa ngumu kwa sababu Ihefu ndiyo kwanza inacheza Ligi Kuu kwa mara ya kwanza itataka kuonyesha uwezo wake na wamefanya hivyo kwa kutoa upinzani mkubwa kwetu.”

“Kikubwa tumepata ushindi na hii ni mechi ya kwanza, tutaendelea kujiimarika kwa michezo ijayo,” amesema Sven.

Katika mchezo huo Simba SC walitangulia kupata bao kupitia kwa mshambuliaji na nahodha wao John Bocco dakika ya 10 kabla ya Omar Mponda hajaisawazishia Ihefu FC dakika ya 14 na baadae kiungo Mzamiru Yassin akafunga bao la ushindi la Wekundi hao wa Msimbazi dakika ya 42.

JPM: Kitwanga alinisumbua
Mwanasiasa wa upinzani aliyepewa sumu apata fahamu

Comments

comments