Kocha wa Klabu Bingwa Tanzania Bara (VPL) na Kombe la Shirikisho (ASFC) Simba SC Sven Vandenbroeck, amesema ameridhishwa na viwango vya wachezaji wake, baada ya kucheza mchezo mmoja wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Vilat’ O ya Burundi.

Simba walicheza mchezo huo, mwishoni mwa juma lililopita kwenye tamasha la SIMBA DAY, na kikosi chao kilionyesha uwezo mkubwa na kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao sita kwa moja.

Kocha huyo kutoka nchinin Ubelgiji mesema kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake wote aliowatumia siku hiyo, kinampa matumaini ya kuwa na kikosi kipana kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.

“Safu ya ushambuliaji ipo vizuri, nina uhakika wa kumpanga mtu, endapo kutakuwa na mgonjwa au kutumikia adhabu basi sitapata wakati mgumu wa kuumiza kichwa,” amesema Sven na kuongeza.

“Kutakuwa na ushindani mkubwa wa namba, jambo ambalo litasababisha kuumiza kichwa kufikiri nimwanzishe nani, hii ndiyo maana ya kikosi kipana kwa timu mchezaji anayetoka na anayeingia kuwa na uwezo mkubwa.”

Katika mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki, kikosi kilichoanza dhidi ya Vital’O kilishinda mabao mawili kwa sifuri  hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza, na baada ya mapumziko Sven alibadili kikosi kizima, ambapo kilichoingia kilicheka na nyavu mara nne na kuifanya Simba kushinda mabao sita kwa sifuri.

Katika safu ya ulinzi iliyoanza, ilikuwa chini ya mabeki wa kati wapya mzawa Ibrahim Ame na Mkenya Joash Onyango ambao walionyesha kuelewana vizuri, huku kiungo mchezaji mpya, Mzambia Larry Bwalya akifanya makubwa wakati mshambuliaji aliyesajiliwa akitokea KMC, Charles Illamfya na Mkongomani aliyetokea Lusaka Dynamos, Chris Mugalu kila mmoja akicheka na nyavu mara moja, hali inayoonyesha itaongeza ushindani wa namba dhidi ya John Bocco na Meddie Kagere.

Simba SC mwishoni mwa juma hili watacheza mchezo wa kuwnaia Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo FC mjini Arusha, na mwishoni mwa juma lijalo wataanza harakati za kutetea taji la Ligi Kuu Tanzania Bara Msimu wa 2020/21.

Azam FC Waboresha mikataba benchi la ufundi
Hii hapa Dodoma jiji FC ya 2020/21