Mara baada ya Kanye west kutua nchini Uganda studio maarufu nchini humo zilipata baraka za kumpokea ‘rapper’ Kanye west na kufanya nae kazi kwa siku tano, Swagz avenue wameshiriki vyema kuipika ”Yandh “.

Kwenye waraka wao ambao wameuachia kwenye kurasa zao za kijamii, wamesema kuwa kazi ilianza punde mara tu baada ya Kanye West kuwasili nchini Uganda.

“Production work started the moment he arrived. Working with Kanye West for the 5 days while he was here open our eyes on how we doing business and our perception on music at a global level”.

”Kazi ya utayarishaji ilianza alipowasili tu nchini Uganda. Siku 5 tulizofanya kazi na Kanye West ametufungua macho yetu namna ya kufanya biashara ya muziki utakaokubalika duniani kote” Ulisomeka hivyo waraka huo.

Aidha, Kanye west ametaka kufanya nao kazi kwenye Nyanja ya kukuza na kuendeleza vipaji vya muziki Afrika.

Video: Hii ndiyo ndege inayomilikiwa na familia ya kitajiri ya Qatar
Babu Tale: Hawa hajakutwa na tatizo la ini, kama ilivyoripotiwa

Comments

comments