Mwanamuziki Rajab Kahali maarufu Harmonize mapema leo Nov 22, 2021 amehudhuria hafla maalum ya uhifadhi wa mazingira jijini  Dar es salam, hafla iliyoongozwa na mkuu wa mkoa huo Mh. Amos Makala.

Harmonize amempongeza Mh Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake katika kuiimarisha nchi na kuhakikisha mazingira yanakuwa safi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Harmonize amesema kutokana na nafasi yake kama msanii na kioo cha jamii, kuna vijana wengi wenye kumfuatilia hivyo ni jukumu lake kuhamasisha suala la usafi katika jiji la  Dar es salam ili kufikia lengo la serikali katika kuijenga taswira mpya ya jiji hilo.

“Ningependa kuwahimiza vijana kwamba usafi ni suala letu la msingi na najivunia kuwa kati ya vijana wanaohimiza usafi kwani ni haki yetu ya msingi” alisema.

Harmonize ni mmoja wa wasanii kadhaa walioteuliwa kuwa mabalozi wa Usafi na uhifadhi wa Mazingira wa mkoa wa Dar es salaam, wengine ni msanii Ali Kiba pamoja na Steve Nyerere.

Morrison aibwaga Young Africans CAS
Wanaouza Damu dawa inachemka