Muigizaji nguli, Sylvester Stallone anayefahamika pia kwa jina la filamu yake ya ‘Rambo’, ametoa maoni yake kuhusu pambano kati ya bingwa wa zamani wa dunia ambaye hajawahi kushindwa, Floyd Mayweather na bingwa wa mapambano ya UFC, McGregory.

Stallone ameonesha kushangazwa na uandaaji wa pambano hilo akidai kuwa hawakutenda haki kwani anaamini baada ya pambano hilo Mayweather atakuwa akikabiliwa na kesi ya mauaji.

“McGregory ni mpiganaji mzuri na shupavu kwenye ulingo wake (UFC). Lakini Mayweather atakuwa anakabiliwa na kesi ya mauaji baada ya pambano hilo kwa mara ya kwanza. Sio haki,” alisema Stallone.

Aliongeza kuwa waandaaji wa pambano hilo walimpigia simu kabla wakitaka maoni yake kuhusu pambano hilo, lakini aliwajibu kuwa haitakuwa haki hata kidogo kumkutanisha bingwa wa masumbwi duniani ambaye ni ‘genius’ na mtu ambaye hana ujuzi wa mchezo huo.

Alisisitiza kuwa ana heshimu sana uwezo mkubwa wa McGregory na ushupavu wake, lakini ni jambo la ajabu kumkutanisha na Mayweather kwenye ulingo wa ndondi na wakategemea atafanya kitu cha ajabu.

Mayweather na McGregory wanatarajia kupanda ulingoni August 26 mwaka huu kukata mzizi wa fitina, Las Vegas, Marekani, pambano ambalo limeandaliwa na kampuni ya Mayweather (Mayweather Promotion).

Singida United yapania kufanya makubwa VPL
Magazeti ya Tanzania leo Juni 18, 2017