Shirika la Uchunguzi wa Silaha za Kikemikali la Umoja wa Mataifa limepewa kibali cha kufanya uchunguzi katika eneo la Douma nchini Syria.

Kundi hilo la wataalam liliwasili jijini Damascus Ijumaa wiki hii, lakini walishindwa kuingia katika eneo la Douma kwa sababu zilizotajwa na Syria na Urusi kuwa ni za kiusalama.

Kutokana na hatua hiyo, Marekani na washirika wake Uingereza na Ufaransa waliibua tuhuma kuwa Urusi imeweka kizuizi hicho ili kusaidia kuficha ushahidi wa tukio hilo kwa lengo la kuisaidia Syria dhidi ya mkono wa sheria za kimataifa.

Syria imeendea kusisitiza kuwa tukio la shambulizi la silaha za kemikali katika eneo hilo lilitengenezwa na Marekani kwa kushirikiana na waasi kwa lengo la kupata sababu za kuingia nchini humo kufanya mashambulizi.

Ripoti imeeleza kuwa zaidi ya watu 40 walipoteza maisha ikiwa ni pamoja na watoto baada ya ndege kudondosha mabomu yenye sumu ya kemikali katika mji wa Douma wakati ambapo bado ulikuwa unadhibitiwa na waasi.

Marekani na washirika wake walifanya mashambulizi makali, wakipiga makombora 100 katika maeneo waliyodai kuna maghala ya silaha hizo za kikemikali.

Urusi imeendelea kupinga vikali hatua hiyo ya Marekani na washirika wake kwa kueleza kuwa imefanya uonevu na kuvunja sheria za kimataifa kwa kuiadhibu Syria wakati bado uchunguzi haujafanyika.

 

Michy Batshuayi kukosa michezo iliyosalia Ujerumani
Video: Mambosasa azungumzia kuhusu kukamatwa kwa Diamond, Nandy, Bill Nas na Hamissa Mobeto