Rapa T.I amezungumzia mpango wa Serikali ya Marekani kuweka sheria kali inayobana umiliki wa silaha za moto kutokana na mauaji ya kutumia silaha dhidi ya halaiki ya watu nchini humo, ambapo hivi karibuni shule ya Douglas imekuwa mfano.

T.I ameiambia TMZ kuwa anaamini inapaswa kuwa na vikwazo vya hali ya juu kwa umiliki wa silaha kwa watu ambao wana matatizo ya akili. Lakini alieleza kuwa ana hofu kama raia watanyang’anywa silaha, Serikali inaweza kuwageuza watumwa.

“Ninahisi kama mtu atapoteza haki ya kumiliki silaha kama mwananchi, unairahisishia Serikali kuwageuza wananchi watumwa, wanapokuwa hawana haki ya kuwa na silaha za moto,” alisema T.I.

Rapa huyo ni mmoja kati ya watu waliowahi kushtakiwa kwa makosa ya kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Mkali huyo wa ‘Live Your Life’ alisema kuwa anachokiona sasa kama tatizo zaidi ni mpasuko au ubovu wa mfumo wa uongozi.

Alichoamua Mutungi maandamano ya Chadema yaliyomsababishia kifo Akwilina
Drake kuwatosa Jordan, apeleka majeshi Adidas