Mwaka huu umeisha vibaya kwa wanandoa maarufu nchini Marekani, rapa T.I na mkewe Tiny ambao wamevunja ndoa yao iliyodumu kwa miaka sita.

Imeelezwa kuwa Tiny alifungua jalada la talaka mahakamani dhidi ya mumewe huyo ikiwa miezi michache imepita tangu wampate mtoto wao wa kike waliyemuita Heiress.

Taarifa za madai ya talaka hiyo zimekuja ikiwa ni wiki chache zimepita baada ya Tiny kuonekana akiwa na bondia Floyd Mayweather kwenye sherehe ya Halloween ya Mariah Carey.

Picha zilizowekwa kwenye akaunti moja ya Facebook inayotumia jina la Tiny ilimuonesha Mayweather akiwa amemuwekea mkono mke huyo halali wa T.I, hali iliyozua uvumi kuwa huenda ‘walifanya yao’.

T.I alikuwa na uhasama wa muda mrefu na Mayweather kuhusu mkewe Tiny akimtuhumu kwa kuingilia ndoa yake. Uhasama wao ulifikia hatua ya kutishiana kutwangana ngumi huku Mayweather akionesha kushindwa kukaa mbali na Tiny kila walipokutana kwenye matukio mbalimbali, hali iliyoendeleza chuki.

T.I (36) na Tiny (41) walikuwa katika uhusiano tangu mwaka 2001 na wakafunga ndoa Julai 30 mwaka 2010 huko Miami Beach, California nchini Marekani.

Wawili hao wamebarikiwa kuwa na watoto wawili wa kiume, King Harris (12) na Philant Harris (8) na mtoto mmoja wa kike waliyempata Mwezi Machi mwaka huu.

Video: Majaliwa awasha moto, ataka jibu, Nyoka wa maajabu afa na mtu wake
Majaliwa ageukia malipo ya wakulima