Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limeongeza idadi ya wachezaji wa akiba kutoka 7 hadi 9 kuanzia hatua ya Robo Fainali itakayochezwa tarehe 14 Mei, 2021.

Aidha kuhusiana na idadi ya wachezaji watakaoingia kwenye mechi moja CAF wanasema vilabu vitataarifiwa hivi karibuni baada ya marekebisho yanayotarajiwa kufanywa na FIFA kupitia IFAB (International Football Association Board) ambao wanahusika na marekebisho ya sheria na kanuni.

USHIRIKI WA MASHINDANO

Mashirikisho/Vyama vya Soka vya Nchi vimetaarifiwa kuviambia vilabu vitakavyoshiriki Mashindano yajayo ya CAF (Inter club Competitions) kwa msimu wa 2021/2022. Kwamba wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kwa Kamati ya Mashindano ya CAF kupitia CMS (Competition Management System) sio zaidi ya tarehe 30 Juni, 2021.

USAJILI WA WACHEZAJI

Usajili wa wachezaji mwisho ni Julai 10 bila faini. Kipindi cha pili ni kati ya Julai 11 na Julai 20 kwa faini ya Dola za Marekani 250 (Usd 250) kwa mchezaji mmoja. Aidha kipindi cha tatu ni kuanzia Julai 21 hadi Julai 31 ambapo Vyama vya soka haviruhusiwi kuondoa jina la mchezaji yoyote bali kuongeza mapya huku faini ikiwa Usd 500 kwa mchezaji mmoja na hawa wataanza kutumika katika hatua ya pili ya raundi za mwanzo na kuendelea.

LESENI ZA MAKOCHA Kocha mkuu lazima awe na Leseni A ya CAF na au Pro-License, huku Kocha msaidizi lazima awe na Leseni B ya CAF na kuendelea. Hii ni kwa mashindano yote yani CAFCL &CAFCC.

Simbachawene: Kitambulisho cha NIDA sio uraia
PICHA: Rais Samia awasili Kenya, akagua gwaride