Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Njombe imefanya oparesheni ya dharura ya ukaguzi wa mashine za Kielektroniki za kukatia risiti katika taasisi za shule, Zahanati pamoja na vituo vya afya na kubaini kuwa idadi kubwa ya taasisi hizo hazitumii mashine hizo.

Hayo yamesemwa na Meneja wa TRA mkoa wa Njombe, Musib Shabani, ambapo amesema kuwa katika uchunguzi mdogo uliofanyika wamebaini kuwa kumekuwa na ukwepaji mkubwa wa ulipaji kodi za mapato katika taasisi binafsi za shule na afya.

Amesema kuwa wamiliki wengi wamekuwa wakikwepa matumizi ya mashine za kielektroniki kwa madai ya kukosa elimu juu matumizi ya EFD katika taasisi hizo jambo ambalo halina ukweli na kuagiza ifikapo machi mosi kila mmiliki wa taaisisi hizo awe amenunua mashine hizo.

Aidha, wakitoa utetezi wao mara baada ya kubainika kutotumia mashine za EFD baadhi ya wamiliki na wakuu wa shule akiwemo Anna Mwalongo ambaye ni mkurugenzi wa Hagafilo Holdings pamoja na Andrew Chikwanda mkurugenzi wa GILGAL wamesema kuwa sababu kubwa ya kutotumia mashine hizo ni uelewa mdogo .

Hata hivyo, licha ya kubainika kuwa taasisi nyingi za biashara hazitumii EFD, lakini baadhi ya watumiaji wamesema mashine hizo zimekuwa na dosari kubwa na kutoa mapendekezo kwa serikali kuhakikisha zinarekebishwa kwa wakati.

Video: Mnyukano Lugola, Tundu Lissu, Sababu 3 mauaji ya watoto Njombe
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Februari 15, 2019

Comments

comments