Katika kuadhimisha Siku ya Moyo Duniani tarehe 29/09/2021 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Wilaya ya Kigamboni watafanya upimaji wa magonjwa ya Moyo bila malipo kuanzia sa 2 asubuhi

Upimaji huu utawagusa zaidi wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa jirani na wahusika ni watoto na watu wazima ambapo kutakua na wataalamu wa Lishe watakaotoa elimu ya ulaji bora kwa afya ya moyo.

KWa Wananchi watakaokutwa na matatizo ya moyo watapewa rufaa ya kwenda kuchunguzwa zaidi katika hospitali ya Muhimbili kitengo cha moyo cha JKIC

Katika maadhimisho hayo wananchi watapimwa magonjwa ya ziada kama Shinikizo la damu, Sukari, Uzito na Urefu, na mfumo wa umeme wa moyo.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya Moyo mwaka huu ni “Tunza Afya ya Moyo wako ili utunze maisha ya Wengine”

Wizara ya ardhi kuhamasisha chanjo Uviko 19
Benki ya Dunia kuinua uchumi wa Tanzania