Baadhi ya wananchi mjini Tarime mkoani Mara wamekuwa hawalipi Ankara za maji kwa wakati, huku Taasisi za Umma zikiwa zinaongoza kwa madeni yenye jumla ya shilimgi Milinoni 13,092,625.50 deni la Mwezi mmoja jambo linalokwamisha utendaji kazi wa Mamlaka ya Maji .
 
Hayo yamesemwa na Meneja wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Tarime, Passian Martin katika kikao cha uzinduzi wa Bodi ya maji mjini humo, ambapo amesema kuwa deni hilo ni la mwezi Machi, 2019.
 
Amezitaja Taasisi hizo za Umma kuwa ni Jeshi la Magereza linadaiwa Milioni 5,311,131.00, Tarime Teachers Collage (TTC) inadaiwa kiasi cha Milioni 1,046,005.00, Hospital ya Halmashauri ya Mji wa Tarime Million 4,178,431.00, Tarime Sekondari Laki 148,874.00, 27 KJ-Rest House 204,300.00, 27 KJ 100,635.00.
 
Zingine ni RPC (Tarime/Rorya) 69,574.00, RPC Tarime – Police Line 436,017.00, RPC Tarime- Canteen 660,734.00, RPC Tarime-Kikosi cha Mbwa 316,671.50, S/M Buhemba Mazoezi 80,175.00, NTC Tarime 228,078.00, Bomani Sekondari 210,000.00 na TTC Rest House 102,000.00.
 
Ameongeza kuwa mbali na madeni hayo Mamlaka ya maji inakabiliwa na changamoto zikiwemo za kutokuwa na dira za maji kwa zaidi ya 40% ya wateja waliounganishiwa maji, hivyo gharama za malipo kutoendana na matumizi halisi ya maji.
 
“Tukifuatilia madeni tunaambiwa wanategemea pesa kutoka hazina sasa utakatia hospitali maji! pia hatuna mfumo wa kielektroniki utakaowezesha kutoa Ankra kwa wakati na kuongeza uwezo wa kukusanya mapato, mfumo wa Umeme uliopo ni Luku hivyo, Mamlaka kulazimika kununua umeme kwa gharama kubwa tofauti na mwongozo unavyosema gharama za umeme zitalipwa na Wizara ya Maji,”amesema Martin.
 
Aidha, amesema kuwa Mamlaka hiyo inakabiliwa na ukosefu wa chanzo cha maji cha kudumu ili kutosheleza mahitaji na mita kuchafuka kutokana na kutokuwepo ubora wa maji hivyo kufanya usomaji wa mita kuwa mgumu.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya Bodi ya Maji, Sinda Sabega ambaye ni Diwani Kata ya Nyandoto (CCM) aliitaka Mamlaka kuzipa Taasisi muda wa siku 14 ziwe zimelipa madeni vinginevyo zikatiwe huduma ya Maji huku akiitaka Mamlaka kutoa orodha ya madeni ya Wananchi ili iwe rahisi kufatilia.
 
Mwenyekiti wa kamati ya Fedha Bodi ya maji, Calvin Mwasha ambaye ni Mganga mkuu wa Halmashauri ya mji wa Tarime yeye aliahidi wiki mbili deni la hospitali litakuwa limelipwa kwa kile alichosema hawezi kuwa mjumbe wa bodi halafu hospitali idaiwe

Takukuru yatoa elimu kuhusu Rushwa mkoani Lindi
Nyoka weusi wamuondoa Rais Weah ofisini, wapotea