Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako kupitia tangazo la Serikali namba 697 la Novemba 25, 2022 ametangaza Kima cha chini cha mshahara wa wafanyakazi kwa sekta binafsi kitakachoanza kutumika Januari mosi, 2023.

Kima hicho kimeainisha sekta 12 za kilimo, afya, mawasiliano, kazi za majumbani na hotelini, huduma za ulinzi binafsi, nishati, usafirishaji, ujenzi, madini, shule binafsi na sekta ya biashara na viwanda, huku sekta ya uvuvi na huduma za baharini wakiwa na kima cha chini cha Shilingi 238,000 kwa mwezi na sekta nyingine zote ambazo hazijaainishwa katika tangazo hilo wakilipwa Shilingi 150,000 kwa mwezi.

Tangazo hilo limekuja miezi mitano kupita, tangu Waziri Ndalichako kutangaza kuwa Serikali ilikuwa katika hatua za mwisho za kutangaza kima cha chini kwa Sekta binafsi, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 63 wa Chama cha Waajiri na kwamba mfanyakazi wa migahawa, nyumba za kulala wageni na baa atalipwa kima cha chini cha Shilingi 150,000 kwa mwezi, hoteli za kati Shilingi 180,000 na hoteli za kitalii Shilingi 300,000.

Kuhusu Wafanyakazi wanaofanya kazi katika huduma za mawasiliano wao watalipwa kima cha chini cha Shilingi 500,000, wakati wafanyakazi wa huduma za utangazaji na vyombo vya habari, Posta na usafirishaji wa vifurushi wao watalipwa kima cha chini cha Shilingi 225,000.

Aidha, katika sekta ya madini, wenye leseni za uchimbaji na utafutaji madini wao kima cha chini cha mshahara kitakuwa Shilingi 500,000, huku wenye leseni za wachimbaji wadogo ni Shilingi 300,000 na wenye leseni za wafanyabiashara kikiwa Shilingi 450,000 wakati huduma za shule binafsi kuanzia shule za awali, msingi na sekondari watalipwa kima cha chini Shilingi 207,000, sekta ya biashara na viwanda wakilipwa Shilingi 150,000 na Taasisi za fedha wakilipwa Shilingi 592,000 kwa mwezi.

Kwa upande wa sekta ya Nishati makampuni ya kimataifa watalipwa Shilingi 592,000, makampuni madogo Shilingi 225,000, na sekta ya usafirishaji katika huduma za usafiri wa anga watalipwa Shilingi 390,000 huku sekta ya Nishati makampuni ya kimataifa wakilipwa Shilingi 592,000, makampuni madogo Shilingi 225,000, sekta ya usafirishaji, huduma za usafiri wa anga watalipwa Shilingi 390,000.

TAWA yatekeleza agizo la Rais udhibiti wanyama wakali, waharibifu
Mabadikiko hali ya hewa yanavyoathiri haki za Binadamu