Hapa chini nimekuandikia tabia za wanaume ambazo zinawachukiza wanawake.

1. Wanaojiona Kama Wafalme (King Husband).

HIi ni aina ya wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na hupenda kuwafanya wake zao kuwa kama watumwa. Hawafanyi chochote ndani ya nyumba kazi yao ni kutumatuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kupika, wanataka waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosea kidogo ni maneno au kipigo. Mwanamke hana kauli ndani na mume akiingia nyumbani ni kama bosi anavyoingia ofisini, wote kimya hakuna hata kuongea.

2. Wanaume Wanaojihisi Bado Hawajaoa (Bachelor Husband). Hii ni aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa chochote. Hufanya mambo kama vile bado hawajaoa, hutumia muda wao mwingi na marafiki zao wakifanya mambo ambayo mke hata hayajui mke anaweza kustukizia tu mume kanunua gari bila kumshirikisha na mume haonyeshi hata kujali kuweza kumshirikisha.

3. Wanaume Wenye Gubu (Acidic Husband). Hawa hukasirika kila mara tena bila kua na sababu ya misngi, mambo hayaishi, kosa la mwaka juzi anaweza kukukasirikia leo.

4. Mume Wa Kila Mtu (Genarel Husband). Hawa wanajifanya wasamaria wema, wanajali kila mwanamke, wanajali marafiki wakike wa mke na wakwao kuliko wanavyowajali wake zao. Mke anaweza kuwa na shida akasema hana hela lakini rafiki akampa. Wana marafiki wengi wakike na mara nyingi huwa hawaachani kabisa na ma X wao, wakiwalalamikia wanawasaidia kuliko hata wanavyowasidia wake zao wakati wakiwa na shida.

5. Wanaume Wanaojifanya Wagumu (Dry Husband). Hawa wanajifanya wagumu sana, hawana yale mambo ya kimahaba na wao hujua kuwa ndoa ni kuleta chakula tu na kushughulika kitandani.

6. Wanaume Wanaopenda Kutumia Wake Zao (Panadol Husband). Hawa huwa wanaume pale tu wanapokuwa na shida, wanakuwa na wake wazuri wanaowajali lakini wao wala hawajali.

7. Wanaume Ambao Hawataki Kukua (Baby Husband). Bado wanatabia za kitoto, hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe mpaka kuuliza kwa ndugu zao, mtu kaoa lakini kila siku humpigia simu Mama yake kuuliza hiki na kile.

8. Mume Mtalii (Visiting Husband). Hawa wanakuja nyumbani kama wageni vile, mume ataihudumia familia yake kwa kila kitu lakini hawezi kuipa muda wake. Akirudi mke na watoto wamelala ni kugonga na hana sababu za msingi za kuchelewa, hata mwisho wawiki hupenda kutumia na marafiki au ndugu lakini si na mke.

9. Wanaume Wanaofuatilia Kila Kitu (Stalking Husband). Hii ni aina ya wanaume ambao hufuatilia kila kitu, huchunguza kila kitu mwanamke anachofanya na hawampi pumzi. Akienda sehemu atachunguza anaenda na nani na alikutana na nani, huwa na wivu wa ajabu ajabu na kila saa huhisi wake zao ni wasaliti.

10. Mwanaume Mbahili (Miserly Husband). Huyu anaweza kuwa na hela lakini mbahili ajabu. Akimpa mwanamke hela atafuatilia matumizi yake mpaka senti ya mwisho, anafuatilia mpaka mambo ya jikoni.

Mchimbaji wa Madini afariki kwa kukosa hewa
Rais Shein asamehe wafungwa 19

Comments

comments