Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) kimeingia mkataba na Kampuni ya DataVision International kutoa huduma ya ukataji wa tiketi za mabasi kwa njia ya elektroniki.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa TABOA, Ennea Mrutu ambapo amesema kuwa hatua hiyo itaokoa mamilioni ya fedha ambayo yamekuwa yakipotelea kwenye mikono ya wapiga debe.

“Tumefanya mazungumzo na wenzetu wa kampuni ya DataVision International kwa ajili ya kuanza kutukatia tiketi kwa njia ya elektroniki ambayo tunaona ni sahihi kabisa, tunafanya hivi kwa ajili ya kuokoa fedha nyingi ambazo zimekuwa zikipotelea mikononi mwa wapiga debe,” amesema Mrutu

Aidha, amesema kuwa tayari DataVision imeshapata baraka zote ndani mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika mwishoni mwa wiki hii, ambapo wamiliki wengi wamekubalia na maelezo yaliyotolewa na kampuni hiyo juu ya fedha zinazopotea.

Kwa upande wake, Naibu Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, William Mgaya Kihula amesema kuwa njia hiyo itawasaidia wamiliki kuokoa mamilioni ya fedha zao ambazo zimekuwa zikipotelea kwa wapiga debe.

DataVision International ni kampuni ya kizawa iliyopo Mikocheni jijini Dar es salaam ambayo inajishughulisha na masuala ya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Tafiti, Malipo ya Kadi pamoja na Mafunzo ya Kitaalam.

 

 

Eminem afunguka kuhusu kupondwa kwa albam yake ‘Revival’
Watoto ombaomba kuchukuliwa hatua kali kisheria

Comments

comments