Mtandao wa Asasi za Kiraia wa Kuangalia Uchaguzi Tanzania (TACCEO) imeotoa ripoti yake kuhusu uchaguzi Mkuu visiwani Zanzibar na kutoa mapendekezo yao.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TACCEO, Israel Ilunde alisema kuwa matokeo ya uchaguzi huo ni halali hivyo wanaitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.

“Sasa sisi tunaitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar iweze kufikiria upya uamuzi wake… sasa sijui ni uamuzi wa Mwenyekiti yule ama ni uamuzi wa Tume. Wakakikishe kwamba wanatangaza matokeo ili tuweze kumfahamu na kuepusha gharama ambazo sio za lazima [kurudia uchaguzi] na kuepusha vurugu ambazo zinaweza kutokana na ukimya unaoendelea na hiyo makusudi inayofanyika,” alisema Ilunde.

Katika hatua nyingine, mtandao huo pia ulieleza kuwa ulibaini kuwepo kwa unyanyasaji wa kijinsia katika ngazi mbalimbali wakati wa uchaguzi huo zikiwalenga zaidi wanawake.

Alisema kuwa walibaini kuwa asilimia 9 walivamiwa kwa maneno ya kashfa, asilimia 2 walihangaishwa na Polisi na asilimia 5 walifanyiwa unyanyasaji majumbani.

Mwenyekiti huyo wa TACCEO aliongeza kuwa wapiga kura hawakuwa na elimu ya kutosha ya uraia ingawa walijitokeza kwa wingi kupiga kura na kwamba kulikuwa na ukandamizaji uliofanywa na vyombo vya dola kwa Asasi za Kirai zilizokuwa zikifuatilia uchaguzi huo. Alieleza kuwa wao ni moja kati ya waathirika kwani vifaa vyao vya kufanyia kazi vilishikiliwa na Polisi siku ya uchaguzi na kwamba bado hawajarudishiwa.

 

Magufuli azilipua taasisi zilizotumia mabilioni angani
Ukawa waeleza sababu za kuzomea Bungeni Na Watakachofanya Baadae