Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetoa wito kwa wakulima na wasindikaji wa zao la Mahindi kuwekeza katika teknolojia za kisasa kwa lengo la kuzuia upotevu wa mahindi baada ya kuvunwa ili kuleta tija katika mnyororo wa thamani wa zao hilo.

Hayo yamesema na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara, Augustino Matutu Chacha wakati akizungumza na wawekezaji katika usindikaji wa zao la mahindi mara baada ya kuzindua mradi maalum wenye lengo la kuchagiza wawekezaji hao katika uongezaji wa thamani wa zao hilo.

“Natoa wito kwa wasindikaji kutumia fursa za mradi huu ili kuongea tija katika shughuli zao kwakuwa mradi huu utakuwa salama kwa wakulima,” amesema Chacha.

Kwa upande wake Msimamizi wa mradi huo, Eunice Mbando amesema kuwa mfuko huo umelenga kuwajengea uwezo wasindikaji wa ndao kuwa sehemu ya uongezaji wa thamani wa mnyororo wa zao hilo.

Akizungumza kwa niaba ya wasindikaji walioshiriki katika uzinduzi wa Mradi huo, Savior Chanay kutoka Kampuni ya Real World ya mkoani Ruvuma ameishukuru Serikali kupitia TADB kwa kuja na Mradi huo ambao utaongeza tija katika mnyororo wa thamani wa mahindi.

 

Video: Chadema wapaza sauti kuhusu Sugu, 'Mwacheni awatumikie wananchi wake'
Habari Picha: JPM aitembelea familia ya Dkt. Kigwangala kwaajili ya kutoa pole