Leo ni siku ambayo baadhi ya maeneo Duniani yanaadhimisha siku ya Kupinga matumizi ya Tumbaku.

Ambapo tafiti zinasema uvutaji wa tumbaku huchagiza asilimia 40 ya magonjwa ya kansa na asilimia 30 ya magonjwa ya moyo.

Katika tafiti zilizofanyika zimeeleza kuwa wagonjwa wa kansa iliyotokana uvutaji tumbaku kwa asilimia kubwa hufariki dunia ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

Watu wanaotumia bidhaa zenye tumbaku wanahatari kubwa kutokana na moshi wanaouvuta kwani unakuwa na kemikali nyingi ambazo hudhuru vina saba (DNA) ambayo hupelekea kansa.

Na katika maadhimisho ya siku ya kupinga matumizi ya Tumbaku dunia imelenga kutoa elimu katika jamii juu ya magonjwa ya moyo yanayotokana na Tumbaku.

Matumizi ya Tumbaku husababisha aina tofauti tofauti za kansa ikiwemo kansa ya koo, kansa ya mapafu, kansa ya mdomo, kansa ya kibofu, kansa ya ini, kansa ya figo, kansa ya utumbo, kansa ya kizazi, aidha watu wasiovuta moshi wa tumbaku ambao hawa hutatafuna wapo hatarini kupata kansa ya mdomo, ulimi, mashavu na kansa ya mifupa ya taya.

Aidha katika tafiti zilizofanyika na waatalamu wamebaini mambo yafuatayo.

  1. Vifo vya watu milioni moja nchini India husababishwa na matumizi ya Tumbaku.
  2. Kila baada ya sekundi 6 mtumiaji wa tumbaku hufariki dunia
  3. Moshi wa Tumbaku una Zaidi ya kemikali 4000 ambapo kemikali 250 ni hatari kwa afya ya binadamu na kemikali 50 zimebeba vimelea vinavyosababisha kansa.

Lakini pia siku hii ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani ni vyema ukafahamu umuhimu wa kuacha kutumia zao hilo.

  1. Huokoa pesa
  2. Hufanya mzunguko wa damu kuwa sawa/ hali ya kawaida
  3. Kujiepusha na magonjwa ya moyo, kansa na mengineyo.
  4. Huweka sawa uwezo wa uzalishaji
  5. Hufanya ngozi na meno yako kuwa vyenye afya

 

 

 

 

 

Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Nigeria
Lampard ala shavu Derby County

Comments

comments