Mtoto kunyonya maziwa ya mama kuna faida nyingi sana ambazo wazazi wa kileo wamekuwa wakipotezea na kuishia kuwanywesha maziwa ya kopo kwa kuhofia kuharibika kwa maumbo yao kutokana na kwamba mama anayenyonyesha anatumia kiwango kikubwa cha chakula ili kutengeneza maziwa ya mtoto lakini pia huofia kuaribu muonekano wa matiti yao.

Kufuatia utafiti uliofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF), unaonyesha kuwa kila mwaka takribani watoto 700,000 nchini hawanyonyeshwi na mama zao hali ambayo inahatarisha afya za wachanga hao.

Lakini pia utafiti mwingine uliofanywa na Takwimu zinaonesha kuwa kuna zaidi ya vifo 85,000 vya watoto wachanga ambavyo husababishwa na kukosa maziwa ya mama.

Pia utafiti uliofanywa na UNICEF umebainisha kuwa wamama wengi katika mataifa au famailia zilizoendelea hawanyonyeshi watoto wao kulinganisha na mataifa na familia zilizo maskini.

Nalo shirika la Afya Duniani (WHO) ilibaini kuwa katika nchi 194 ni asilimia 40 ya watoto waliochini ya miezi sita wananyonyeshwa maziwa ya mama na nchi 23 pekee duniani ndizo zenye kiwango cha unyonyeshaji wa zaidi ya asilimia 60.

Hivyo basi kina mama inapaswa watambue umuhimu wa kunyonyesha watoto wao pindi wakiwa wadogo kwani kumekuwa na tatizo kubwa la kimama kukwepa jukumu hilo hali inayowaletea shida watoto kiafya na kupelekea watoto hao kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara.

Wanasayansi uingereza wamegundua kuwa ukuajia wa ubongo wa mtoto unategemea sana maziwa ya mama na inasaidia kulinda uwezo wa kiakili wa mtoto na wameshauri wamama waache kutumia maziwa ya kopo.

Mtoto anaenyonyeshwa hupata viini lishe na virutubisho vitakavyomfanya akue kiafya, apate kinga ya maradhi kama kuharisha, nakumfanya apone haraka akiugua, na kuzuia kupata kitambi kisicho rasmi (utapiamlo) na pia atakuwa na uzito unaotegemewa katika hali ya lishe bora na kupunguza kudumaa.

Hivyo basi kwa kutomnyonyesha mtoto hasara zake ni kukosa faida tajwa hapo juu.

 

Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Misri
Video: JPM atoa siku 30 kwa wadaiwa JWTZ kulipa, IPTL kwawaka moto