Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa hivi karibuni, waendesha bodaboda wanachangia asilimia 13 ya mimba za utotoni nchini.

Matumizi ya bodaboda, ama pikipiki kwaajili kibiashara, yameongezeka sana Tanzania hasa pale ambapo ni ngumu kupata usafiri mwingine au ufinyu wa barabara, Umaarufu wake unasababishwa na upatikanaji mgumu wa usafiri pamoja na bei nafuu za pikipiki ambazo idadi kubwa huendeshwa na vijana wadogo waliotoka kumaliza elimu ya sekondari.

Tafiti hiyo inaonesha kuwa wasichana wadogo, hasa wale wa vijijini, wapo katika mazingira hatarishi zaidi kushawishika kingono kwa sababu inawabidi kusafiri umbali mrefu kwenda shule. Gazeti la Financial Times linasema, baadhi ya wasichana huishi umbali wa hadi kilometa 15 kutoka shuleni, hivyo huwalazimu kupanda bodaboda badala ya kutembea umbali huo.

Kwakuwa hawana fedha za kutosha kuwalipa waendesha bodaboda hao, huishia kulala nao kama njia ya malipo na kupata ujauzito ambapo hupeleka kufukuzwa shule.

Wasichana kutoka familia masikini ni kundi hatarishi kwasababu ya kiuchumi kunakopelekea kukosa mahitaji yao ya msingi kama kuweza kulipia usafiri, kunawafanya iwe rahisi kunyanyaswa kingono.

Watoto wengi hukumbana na changamoto mbalimbali wanapokuwa njiani kwenda na kutoka shule. Baadhi ya makondakta hukataa kuwachukua kwasababu wanalipa nauli ndogo. Safari ya kwenda na kutoka shule huwaweka watoto katika mazingira hatarishi.

Ripoti ya “Ukatili Dhidi ya Watoto Tanzania” inaonyesha kwamba kati ya wasichana wanne waliotoa taarifa ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia, mmoja kati yao ilimtokea akiwa anaenda shule, aidha kwa usafiri wa umma au akiwa anatembea.

Kwa mujibu wa Ripoti  Ukatili Dhidi ya Watoto Tanzania (2011), msichana 1 kati ya 25 mwenye umri wa miaka 13 hadi 17 amewahi kupewa pesa au zawadi ili afanye ngono. Ripoti hii inaonyesha kwamba asilimia 23 ya wasichana wananyanyaswa kijinsia wakiwa wanaenda au kutoka shule.

Hivyo, madai ya kwamba waendesha bodaboda wanachangia ongezeko la mimba za utotoni nchini Tanzania ni kweli kwa kiasi kikubwa.

Darassa azifungukia tuhuma za kutumia dawa za kulevya, ukimya
UVCCM yakamata gari la Meya wa Jiji