Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ameeleza kuwa na wasiwasi wa hali inayoendelea katika mapigano ya ndani karibu na kiwanda cha nyuklia cha Zaporizhzhia kilichoko kusini mwa nchi ya Ukriane.

Taarifa ya Mkuu huyo wa UN, imetolewa hii leo Agosti 12, 2022 jijini New York, Marekani wakati ambapo kumekuwa na taarifa za matukio ya kutisha yanayoelezewa iwapo yataendelea kuna uwezekano mkubwa wa kuleta maafa.

“Ninatoa wito kwa watu wote wanaohusika kutumia akili na watafute sababu za kutochukua hatua zozote zinazoweza kuhatarisha uadilifu wa kimwili, usalama kwa ujumla na usalama wa kinu cha nyuklia ambacho ni kukubwa zaidi barani ulaya” amesema Guterres.

Amesema, uharibifu wowote utakaotokea katika kiwanda hicho hauta athiri Ukraine pekee, bali unaweza sababisha janga kwa maeneo mengine ya karibu katika ukanda huo na kwingineko na hivyo kutoa wito wa kusitishwa kwa shughuli za kijeshi katika maeneo ya karibu na mtambo huo na kuacha kulenga vifaa vilivyokaribu na mazingira yake.

Guterres ameongeza kuwa, “Ninahimiza kuondolewa kwa wanajeshi na vifaa vyovyote kwenye mtambo huo na kuepuka kupeleka vifaa zaidi au vikosi kwenye eneo hilo. Kituo hicho hakipaswi kutumika kama sehemu ya operesheni yoyote ya kijeshi.”

Hata hivyo, ametaka baada ya kuondoa vikosi vya kijeshi katika eneo hilo la karibu na mitungi ya nyuklia, kufanyike makubaliano ya haraka katika ngazi za kiufundi, ili kuhakikisha usalama wa eneo hilo la kiwanda.

Katika taarifa hiyo, Guterres amehakikisha kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono kikamilifu kazi zinazofanywa na shirika la Kimataifa la nguvu za atomiki IAEA, katika juhudi zake za utendaji kazi salama katika kiwanda hicho cha Zaporizhzhia.

Kenya: Matayarisho makabidhiano Ofisi ya Rais yaanza
Mgogoro wafukuta ujenzi mradi tata wa umeme