Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe ameshambuliwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana wakati akirejea nyumbani kwake jijijini Dodoma.

Mkuu wa idara ya habari ya chama hicho amesema “Ni kweli Mbowe ameshambuliwa. Walimvizia akiwa anapanda ngazi za kwenda nyumbani kwake anapoishi hapa Dodoma, wakamshambulia ameumizwa na sasa amekimbizwa Hospitalini. Taarifa zaidi tutazitoa baadaye.”

Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Gilles Muroto amesema wamepata taarifa kuwa kavunjwa mguu wa kulia na amelazwa Wodi namba 4 hospitalini ya Ntyuka. na ameahidi kutoa taarifa zaidi baadaye.

“Mbowe Amevamiwa na watu watatu, wamemkanyaga kanyaga na kumvunja mguu wa kulia tutatoa taarifa baadaye” Amesema Kamanda Muroto.

Hii siyo mara ya kwanza kwa viongozi wa CHADEMA kushambuliwa Jijini Dodoma kwani Septemba 2017, makamu mwenyekiti Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana nyumbani kwake.

Walichosema waliompiga Mbowe, Kamanda Muroto, Naibu Spika, Mnyika wazungumza
Martin Keown ashauri jambo zito Arsenal