Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ limeendelea kuzuia mashabiki wa soka nchini Tanzania kuingia Uwanja wa Benjamin Mkapa, kwa ajili ya kushuhudia soka la kimataifa likichezwa uwanjani hapo.

‘CAF’ kwa mara ya kwanza iliipiga marufuku mashabiki kuingia uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatua ya Makundi kati ya Simba SC dhidi ya Al Merrikh ya Sudan, uliochezwa mwanzoni mwa mwezi huu.

Safari hii Shirikisho hilo limeendelea na msimamo huo kwa kuzuia mashabiki kuingia uwanjani hapo, kutazama mchezo wa mwisho ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) baina ya Taifa Stars na Libya utakaochezwa Machi 29.

Maamuzi hayo kutoka ‘CAF’ ni hatua ya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 ingawa baadhi ya michezo barani Afrika imepewa ruhusa ya kushuhudiwa na mashabiki viwanjani.

Nigeria ni sehemu ya nchi zilizopewa nafasi ya kuingiza 30% ya mashabiki katika mchezo wake dhidi ya Lesotho.

‘Taifa Stars’ leo inacheza mchezo wa mzunguuko watano wa kundi J dhidi ya Equatorial Guinea mjini Malabo, huku ikihitaji matokeo ya ushindi ama sare kabla ya kucheza nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam Machi 29 dhidi ya Libya.

Dkt. Abbas: Ndoto za Magufuli zitatekelezwa
‘Try Again’: Tunahitaji alama zote tatu