Taifa Stars inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki katika kalenda ya FIFA inayoanza Machi 19 – 27, 2018 dhidi ya timu za Taifa za Algeria na DR Congo.

Stars itasafiri kuelekea jijini Algiers kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji Algeria Machi 22, 2018 na baada ya mchezo huo dhidi ya Algeria, Taifa Stars itarejea nyumbani kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Congo DR Machi 27, 208 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Wakati huo huo timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) imeingia kambini katika Hostel za Makao Makuu ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT Mlalakuwa) kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake AFCON 2018 nchini Ghana.

Twiga Stars itacheza dhidi ya Zambia (She Polopolo) Aprili 4, 2018 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na marudiano kufanyika April 8, 2018 jijini Lusaka nchini Zambia.

Mshindi wa jumla kwa raundi hii atacheza na mshindi kati ya Namibia v Zimbabwe mwezi Mei, na atakayeibuka mshindi atafuzu moja kwa moja kwa Fainali hizo za Wanawake Afrika.

Ngorogoro Heroes kujipima kwa Morocco, Msumbiji
Mganga wa kienyeji mbaroni kwa kumpa bintiye ujauzito