Golikipa wa Timu ya Taifa Tanzania pamoja na klabu ya Mtibwa Sugar, Said Mohamed Said  ‘Ndunda’ amaibuka kidedea katika mashindano ya COSAFA kwa kuchaguliwa kuwa golikipa bora wa michuano hiyo.

Hii ikiwa ni michuano ya 17 ya Kombe la Cosafa, iliyohusisha  nchi wanachama wa Cosafa ambazo ni nchi za Kusini mwa Afrika. Tanzania ikiwa kama moja ya nchi zilizoalikwa katika michuano hiyo.

Said Mohamed ambaye tangu kuanza kwa mashindano ya COSAFA, amedaka mechi moja tu ambayo iliwaibua watanzania kuwa washindi watatu dhidi ya timu ya Lesotho na kushinda mchezo huo kwa magori ya penalt.

Kupitia uwezo aliounesha katika mchuano huo imemfanya atajwe kuwa kipa bora wa michuano ya COSAFA na kupewa tuzo yake, jambo ambalo halikuonekana kwa makipa wengine waliopata bahati ya kudaka mechi zaidi ya moja.

 

NASA wazungumzia afya ya Raila Odinga baada ya kutoka hospitalini
Mtandao haki za binadamu kupinga mahakamani Polisi kuzuia Maandamano