Kocha mkuu wa Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa ametaja majina ya nyota 24 watakaounda kikosi ambacho kitasafiri mwishoni mwa wiki ijayo kwenda Addis Ababa, Ethiopia kucheza na wenyeji wetu kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Oktoba 8, mwaka huu.

Mkwasa maarufu kwa jina la Master amesema wachezaji aliowaita wataingia kambini Oktoba 2, 2016 kabla ya kuanza kukiandaa kuanzia Oktoba 3, 2016 ikiwa mara baada ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya mwishoni mwa wiki hii ambako Mwadui itacheza na Azam huku Mbao ikishindina na JKT Ruvu Oktoba 2, mwaka huu.

Nyota wa Stars walioitwa na Mkwasa ni:

Makipa

Deogratius Munishi (Young Africans), Said Kipao (JKT Ruvu) na Aishi Manula (Azam FC)

Mabeki

Shomari Kapombe ( Azam FC), Juma Abdul ( Young Africans), Vicent Andrew (Young Africans), Mwinyi Haji (Young Africans), Mohamed Hussein (Simba SC), David Mwantika (Azam FC0 na James Josephat (Tanzania Prisons)

Viungo wa Kati

Himid Mao (Azam FC), Mohammed Ibrahim (Simba SC), Jonas Mkude (Simba SC), Muzamiru Yassin (Simba SC)

 

Viungo wa Pembeni

Shiza Kichuya (Simba SC), Simon Msuva (Young Africans), Juma Mahadhi (Young Africans), Jamal Mnyate (Simba SC) na Hassan Kabunda (Mwadui FC)

Washambuliaji

Ibrahim Ajib (Simba SC), John Bocco (Azam FC), Mbwana Samatta (CK Genk ya Ubelgiji), Elius Maguli (Oman), Thomas Ulimwengu ( TP Mazembe Congo)

Mchezo huo utakaofanyika jijini Addis Ababa, umeratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake – Tanzania ni miongoni mwao. Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ethiopia (EFF), wameo

Hii ni faida kwa Tanzania kama itashinda mchezo huo kwa maana kina alama za nyongeza kama inatokea unaifunga timu mwenyeji.

Matokeo ya mchezo huo, ni sehemu malumu kupima viwango vya ubora na uwezo wa timu za taifa. Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 132 kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora. Ethiopia yenyewe inashika nafasi ya 126.

Argentina inaongoza ikifuatiwa na Ubelgiji anakocheza Mbwana Samatta – nyota wa kimataifa wa Tanzania. Samatta anacheza klabu ya K.R.C Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji. Timu nyingine bora kimataifa ni Ujerumani, Colombia na Brazil.

Katika Bara la Afrika, Ivory Coast ambayo ni ya 34 kwa ubora duniani ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na Algeria, Senegal, Tunisia na Ghana.

Kauli Nzito Ya Makocha Serengeti Boys
Bei ya mafuta yaanza kupanda