Meneja wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Benin, utakaochezwa kesho Alkhamis (Oktoba 07) Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Taifa Stars itakuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo huo wa kuwania tiketi ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022, zitakazounguruma nchini Qatar.

Canavaro amesema maandalizi na kila kitu kipo sawa, hivyo ni suala la kusubiri muda wa mchezo huo ambao utashuhudiwa na mashabiki 10,000.

“Kila kitu kipo sawa kwa kuwa tutakuwa nyumbani, tutapambana ili kupata matokeo na tunaamini kwamba ushindani hautakuwa mdogo kwani timu zote zinahitaji matokeo,”

“Jonas Mkude, Bakari Mwamnyeto, Shomari Kapombe na Erasto Nyoni hawatakuwa sehemu ya kikosi kutokana na matatizo mbalimbali.”

“Mkude ana matatizo ya kifamilia huku Kapombe, Nyoni na Mwamnyeto hawa bado hawana utimamu wa mwili (fiti)” amesema Cannavaro

Stars inaongoza msimamo wa Kundi J ikiwa na alama 4 sawa na Benin, huku DR Congo ikishika nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 2 na Madagascar inaburuza mkia wa kundi hilo, baada ya kupoteza michezo miwili.

Twiga Stars kuikabili Zambia
Billioni 50 kujenga bandari ya kilwa